Daniel Patrick Welch - click to return to home page


    English versions 
Arabic versions - Saudi Arabia Catalan versions Croatian versions Czech versions Danish versions Nederlandse versies Finnish versions Versions Françaises Galician versions German versions Greek versions Indonesian articles Le versioni Italiane Japanese versions Urdu versions - Pakistan Polish versions Portuguese articles Romanian versions Russian versions Serbian articles Las versiones Españolas Ukrainian versions Turkish versions

 

 

 

Huyu ni mwanamke Kweli. 
Patricia Jennings-Welch: Mwanamke mkuu, Urithi mkuu

Risala zilizo tayarishwa kupelekwa kwa Kanisa 
la watume la St. Thomas, Peabody Masachusetts, 
Machi 4, 2009
.
mwandishi Daniel Patrick Welch.

(03/09) 

Patricia Jennings-Welch. Salala. Mwanamke wa kikweli! Nilipo jufunza ki moyomoyo, kwa mara ya kwanza mistari kutoka kwa Risala maarufu ya ‘Sojourner Truth’, sikuwacha kufikiria mama yangu. “Yule mtu pale yuasema kwamba wanawake wanahitaji kusaidiwa kupanda magari ya farasi, na kubebwa wavukapo mitaro, na kupewa nafasi nzuri kila pahali. Hakuna mtu anayenisaidia kupanda magari au kuvuka matope, au kunipa nafasi nzuri! Na kwani mimi si mwanamké? Niangalie! Angalia mikono yangu! Nimelima na kupanda, na kuvuna magala, na hakuna mwanamume aliyeweza kunitawala! Na kwani mimi si mwanamke? Niliweza kufanya kazi na kula kama mwanamume – nilipoweza kupata – nakuvumilia viboko pia! Na kwani mimi si mwanamke? Nimezaa watoto kumi na watatu, na nimewaona wote wakiuzwa utumwani, na nilipolia kawa uchungu wa mama, hakuna aliyenisikia isipokuwa Yesu! Na kwani mimi si mwanamke?”

Yote niliyosikia kuhusu heshima na adhama, kuhusu kung’ang’ana na kuepusha wengine kuangushwa, yote haya yatokana na huyu mwanamke wa ajabu la kutatanisha, wa nguvu na hakika la ajabu, ambaye twamuaga kwaheri leo. Mwanamke huyu aliyenifunza kuheshimu nguvu na rehema kwa uzito sawa, mwanamke, aliyenionyesha jinsi ya kuwa mwanamme. Mwanamke huyu aliyenifunza mengine sana, kwa mfano wake nilitabua kwamba hakuna kilicho chini yetu—yakwamba kuzibua misahala ni sawa sawa na kujifunza na kufunza, kusoma au lugha za kigeni, kwamba maisha bila kung’ang’ana ni maisha bila thamani – lakini pia kung’a ng’ana kwa uchoyo bila kuimarisha wengine haina maana na niutozu wa utawa.

Nilikuwa nimebarikika kiajabu kuwa na mahusiano maalum na mwanamke huyu: mama yangu, rafiki yangu, mwandani wangu, mwalimu wangu. Lakini aligusa maisha ya wengi, na kujivunia kikamili maisha aliyoishi pamoja na watoto wake wote, kutokea likizo na safari kwanda San Antonio na Austin mpaka kila mikutano ya kuogelea, ibada, michezo ya mpira, karamu za siku ya kuzaliwa na sherehe alizoweza kwenda, vile alivyoweza kufika huko, kwa mda mrefu alioweza kubaki. Na kupita familia yake ya karibu, watu walijihisi kumiliki kipande kidogo chake. Anaweza kuwa yote haya kwangu, lakini Mima alikuwa raslimali ya taifa katika hali nyingine. Moja la mataraji mengi tuliopata ya onyesha hulka hii pamoja na uwekevu wake mkubwa, tamani lake na kiu ya elimu, na uwezo wake mkubwa wa kufunza. Hulka moja, rafiki yangu Volker kutoka Ugerumani, aliyotuambia nikwamba alikuwa nauwezo wakufanya watu wajisikie wanawe pia: “ alikuwa mama bora zaidi unayeweza kupata. Unavyojua, nilipenda kuchukuliwa kama mmoja wa watoto wake kwa sababu hii: Kila mtu angetaka mwanamke huyu kuwa mamake, kama mwanzisha shule – kama Mensch. Ijapokuwa nihuzuni ametuacha sasa, atakuwa hai zaidi ya watu wengi waliohai sasa, katika fahamu zetu.”

Hii ndiyo sababu hakuna maua: yanawakilisha mbegu zote alizopanda, maua yote yaliyomea, watu wote ambao maisha na ndoto zao alizitiamoto, sukuma, imarisha, zalisha, okoa au kufanywa tajiri kidogo kwa sababu ya kumjua mwanamke huyu.

Katika mistari hii, nitakuwa ajizi nisipomtaja bibi yangu Julia, ambaye ni mwenzi wangu katika kina cha huzuni langu kama alivyo katika mambo yote mengine. Amekua na mimi kwa miaka mingi, kunisaidia kumhudumia mama yangu, kama wengi wenu mjuavyo, amekua mjogwa miaka mingi. Kutoka kumsaidia kuoga, na kuvaa siku ya ndoa yetu, mpaka wakati wa mwisho ma maisha ya mama huyu mkuu, mapenzi na msaada wa Julia, kwangu, kwa mama yangu, kwa ndoto tulizogawa—Sisi nondo watatu wa ishara za kinajimu za kichina au timu ya PD&J, kama alivyosema alipokuwa amekaribia kufa, mapenzi tuliyohisi pamoja walikuwa yakushikika na kupasa.

Na ijapokuwa nyakati zingine alikuwa na mahitaji mengi, tunapaswa kukumbuka sasa ilikuwa kwa sababu ya mapenzi yote haya alitarajia yaliyobora. Ubeti mmoja kutoka kwa wimbo tulioimba mbeleni niwakusisimua sana – Nilizaliwa huko bondeni/ ambako jua lakataa kuwaka/ lakini napanda huko kuliko juu/ nitaufanya mlima huo wangu!

Na bila shaka, alitarajia hili kutoka kwa kila mmoja — ujuwe au la. Ni sifa bora zaidi ya mwalimu... na pengine ya mama pia. Na wakati mwengine aliwakaazia wale watu waliosema hawawezi na hasa wale ambao wengine walisema hawataweza. Waona, fumbo alilokuwa Pat Welch, daima kuweka malengo yake juu zaidi (kwa sababu wakati wengine walifanyika) na kuwa na upande wa ubithi pia: Haikuwa kwamba kujionea huruma ilikuwa ni vibaya – ilikuwa tu kikwazo sana. Mara ngapi katika hizi wiki zilizopita watu wametukujia na tamthilia, kama yule mama aliyetuambia, Julia na mimi, “Nilipokuja kumleta mwanangu shuleni, nilimwambia mamako ‘siwezi kuja kumchukua baadaye,’ alisema ‘ wewe mpeleke shule tu; tuta tafuta mbinu.’” Nitafanya mlima ule wangu! Lakini tena, bila kusahau kuwaimarisha wanizungukao pia.

Mmoja wa mabinamu wangu aliandika ya kwamba ‘ sote tulipata changa moto nyingi kutoka kwa shangazi Pat. Alikuwa na namna ya ajabu yakuona mazuri na hakukuwa na lolote gumu kupita kiasi lisiloweza kufanyika mara anzapo kulifanya. Na nadhania aliweza kuwashawishi wengi waliweza kufanya mambo hawange jaribu.’ Kwa uhakika, sifa hii ya kung’ang’ana thidi ya vikwazo vyovyote iliwacha tatizo la kushangaza popote alipoenda. Nilikuwa nimeandika mbio mbio tarehe makosa nilipotuma barua ya mazishi. Nikatuma sahihisho rahisi chini ya kichwa “kosa.” Binamu yake aliniandikia haraka kuniambia kwamba alitumai kwamba yote ilikuwa kosa. “Patsy alisema yote ilikuwa kosa tu na alikuwa haendi popote!”

Wiki kadhaa kabla ya kufa alinigeukia na kusema “Mwanangu nataka uniweke kwa coma. Halafu wataniamsha miaka tano au kumi watakapo pata dawa ya yote yanayo nithidi.” Rafiki wengine aliuliza kwamba, vile alielekea dukani, angemletea chochote. “ Pengine kama unaweza kuniletea jozi la mapumo,” akatabasamu, na ule mg’aro katika macho yake ya buluu yaliyotuacha twafikiria lazima ywafanya mzaha ... ywafanya mzaha...sindio? haukuweza kujua kwa uhakika...

Alikuwa na shairi alilolipenda sana la baba yake, babu yangu, alilomuandikia. Tulilikariri pamoja katika wiki zake za mwisho, nalilionekana kumpa amani.

Patsy
Leo mwanangu umevalia mavazi meupe
Yanayo mithilisha nasfi ya Mungu
Utembee naye katika yote mazuri
Katika njia aliyotembea Kristo

Mawazo yako safi, mwenendo yako wa nguvu
Ndoto zako zimejazwa tumaini njema
Kukupa nguvu uendelee mbele
Njia ya maisha na mizigo yake uvumilie

Shujaa wa kweli kwa Mungu
Vita vyako ni kwa maisha
Na uwe pamoja na walio mbinguni
Ukimaliza mwendo wako hapa duniani.

Alikuwa ameandika shauri lengine, bila shaka juu ya mama yake na yeye. Hivi majuzi nalifikiria pia katika uhusiano wangu na mama wangu. Tulipokwenda kwa matembezi ya mwisho mwisho, na alisisitiza kuona vitu vyote vilivyokuwa vipya: Lile Y, Danversport iliyojengwa tena, na mwishoni makaburini, na fikiria ilikuwa njia yake yakutuambia alikuwa yajua.

Imani.
Mdharau anaweza dharau, anapopiga magoti na msalaba wake
Akizungusha shanga alizonazo
Lakini amechoka na uchokozi wa maisha
Na anajua tu kwamba amezeeka.

Amechoka na maisha na yuaogopa kifo
Na shanga hizi alizonazo ndio tumaini lake
Kwamba kunakitu baada ya pumzi lepesi la maisha la mwisho
Lisiloonekana na lisilojulikana na sisi.

Na mdharau anaweza dharau, anapobusu msalaba
Na kupiga magoti kichwa kikiinamishwa chini
Yuko na amani na mungu wake, na yeye amefilisika
Na kuchoshwa na vitu asivyoweza kujua.

Y ahora quiero decir algo, aunque brevemente, a la communidad hispana, la que tenia tanto 
amor para mi mama—diciendole simplemente siempre ‘la Dona.’ Y todos supieron de quien 
estabamos hablando, sin tener que decir nada mas. Tan como a muchos otros, la Dona ayudo 
bastante la gente de esta comunidad, con que tenia una connection especial. Me llamo una 
colega anterior desde Santo Domingo para darnos nuestras condolencias, explicando cuanto 
ayudo esta mujer, la dona, una mujer de tanta fuerza, intelegencia y amor, y tambien 
cuanto ayudo a sus hijos y a su familia—diciendo como tantos otros que sentia de Corazon 
que la dona fue, en cualquier parte, tambien su mama a ella. Me recordo tambien, pero no 
es que necesitaba que me recuerden, de la broma que yo siempre hicia con mi mama, 
relajando su pronunciacion en espanol. Zan-a-jor-i-a. Me reganaron, por supuesto, por 
relajar a una mujer con tanta dignidad, y sobre todo que trataba con todo su fuerze a 
conquistar el idioma espanol. Otra Montana que queria subir. Pero ojala, y supongo que 
saben todos, como entendio la Dona, que eso fue todo de amor. 

Ninamuomba msamaha Padri Sherridan na nyote hapa kwa kuendelea kupitisha kiasi. Nafikiria ni mbinu ya kunena milele juu ya mwanamke huyu maarufu, kama ubeti wengine wa wimbo tulioimba : Mzishi tafadhali nenda polepole. Lakini wakati ukifika, umefika, na hatutawali saa wala kalenda. Nisameheni. Na sasa, kwa mwanamke huyu mkuu aliyetaka kila wakati kuwa wa mwisho kuondoka karamuni, ni wakati tumeache apumzike. Alipigana thidi ya nasibu, ya ujongwa, ya wakati wenyewe hadi mwisho. Niliinama na kumnog’onezea sikioni mwake alivyokuwa katika kitanda chake karibu kufa, ingawa sina hakika alinisikia tena, kwamba mambo yalikuwa sawa, yakuwa anaweza kupumzika sasa bila kuchoka sana. Kulikuwa na tarehe mbili katika wiki hizi zilizopita zinazoeleza tatanishi hili la mwisho. Tarehe 20 januari ilikuwa tarehe ya makutato yake na daktari wa kansa, na ilikuwa baada ya wakati huo tulihisi anatuacha. Na usiku huo, tulipokuwa twalala Julia na mimi juu ya godoro sakafuni katika chumba chake cha kulala, kuwa naye wakati huo mgumu, Nilimdokeza wasiwasi langu Julia, hali. Hasomi, ulia akanijubu. Pat Welch, kunaishara nyingine mbaya zaidi. 

Lakini nakumbuka sasa kwamba januari 20 ilikuwa pia siku ya mzinduo, siku aliyongojea miaka minane mirefu. Na kumbuka dhahiri akilia mwaka 2004; nilipomuliza kanini alisikia uchungu sana, alinijibu, “ lakini sasa pengine sitaishi kumuona Bush akiondoka!” kwa hivyo januari 20 ilikuwa siku muhimu kwake kuliko tulivyo fikiria. Na ile hadithi ya siku nyengine isio ya kawaida niliyovumbua jana. Tulikwenda kwa CVS, ambako tulikwenda mara nyingi kuchukua madawa yaliyosaidia kumweka hai, na sikuweza kuegesha gari bila kulia.

Niliegesha gari katika nafasi ya vilema na nikatoa bango la mamangu bila kufikiria. Nilipogundua nililofanya nilitabasamu, nikifikiria kwamba si yeye wala sheria watani gombeza kwa hatia hii yangu ya mwisho. Lakini nilipoangalia bango lile nyuma ya gari, niliona tarehe imepitishwa : Februari 24, 2009 – siku ileile tuliyomkimbiza Brigham, na safari ya mwisho aliyochukua katika gari letu dogo. Kwa mshangao niliketi na kuwaza. Ni wakati, hatimaye, kumwacha masikini mama huyu apumzike. Pumzika, Ma, pumzika. Twakupenda, na utakuwa daima , daima hai kwetu sisi. « Na njia isimame kukuamkua, na upepo uwe nyuma yako, na jua ling’are joto surani mwako, na mvua inyeshe taratibu shambani mwako --- na mpaka tukutane tena, Mungu akuweke mkononi mwake. Nakupenda Ma. Kwaheri.

Contributions in memory of Patricia Jennings-Welch can be made to The Greenhouse School.

Translation by Baya Mdzomba

^  Top  ^